Jiunge ufaidi miezi 2 bure!

Chodry awafungukia waigizaji wa kike Bongo

Msanii kutoka kiwanda cha Bongo Movie, Diana Nsumba maarufu kama Chodry amesema kuwa waaigizaji wengi wa kike hapa bongo ni washamba sana.

33C5F94800000578-3570857-Leicester_striker_Jamie_Vardy_heads_off_to_training_in_a_white_M-a-31_1462267860274

Diana ambaye anamiliki kampuni ya Twins Film Production ameshafanikiwa kufanya filamu kadhaa ambazo zimefanya poa kama ‘Julieth’, ‘Only You’ na ‘The Same Script’.

Akizungumza na Bongo5, Chodry amesema, ‘Wasanii wengi wa kike wakifanya filamu moja wakitokeza kidogo kwenye cover wanaanza matusi mitandaoni’.

“Mimi huwa nawashangaa sana waigizaji wenzangu, kuna wale ambao wakiwekwa kwenye cover ya filamu mara moja tu wanaanza kujiona na kuanza matusi mitandaoni. Mimi nimeshafanikiwa kufanya kufanya filamu na wasanii kama JB, Hemedy phd, na wengine wengi lakini hata siku moja sijaweza kumdharau mtu. Nawashauri wasanii wenzangu wa kike wenye tabia hiyo tubadilike ndiyo maana filamu zetu zinapanda na kushuka kila siku kwa sababu kama hio za kuridhika mapema wakati bado hatujakipata tunachokitaka,” aliongezea.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW