Burudani

Chris Brown ajutia kichapo alichokitoa kwa Rihanna

Ni zaidi ya miaka nane sasa tangu msanii wa muziki nchini Marekani Chris Brown aachane na mpenzi wake Rihanna baada ya kumtwanga ngumi za kutosha.

Kupitia documentary yake ‘Welcome to My Life’, Chris ameonyesha kujutia kitendo hicho cha kumpiga na kumuumiza Rihanna.

“I remember she tried to kick me, but then I really hit her, with a closed fist, I punched her, I busted her lip. When I saw it, I was in shock. I was like, ‘F*ck, why the hell did I hit her?, From there she just spit in my face … spit blood in my face and it enraged me even more,” ameeleza Chris

Hata hivyo ameongeza kuwa Rihanna alificha funguo ya gari na kusema imepotea na wakatoka nje kuitafuta ndipo mwana dada huyo akaanza kupiga kelele za msaada akidai kuwa Chris anataka kumuua jambo ambalo amelipinga vikali.

Baada ya hapo Chris alijikuta kifungo cha uangalizi wa miaka mitano kwa shabulio hilo na siku 180 za adhabu ya kufanya kazi za kijamii na mwaka mmoja wa ushauri nasaha.

 

 

Na Laila Sued

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents