Burudani

Chris Brown atangaza tarehe mpya ya kutoka kwa album mpya ‘X’, baada ya kuahirishwa tarehe ya mwanzo

Baada ya kushindwa kuitoa katika tarehe iliyopangwa mwanzo hatimaye Chris Brown ametangaza tarehe mpya ya kutoka kwa album yake ya sita ‘X’. Kwa mujibu wa Billboard sasa itatoka November 19.

brezzy
Hapo awali album hiyo ilipangwa kutoka mwezi July lakini ilisogezwa mbele.

Album hiyo itakayokuwa na collabo za mastaa kama Kendrick Lamar, Ludacris pamoja na Nicki Minaj itajumuisha single zake alizotoa mwaka huu ikiwemo ‘Fine China’ aliyoitoa mwezi April, ‘Don’t Think They Know’ pamoja na ‘Love More’ ya hivi karibuni aliyomshirikisha Minaj.

Katika interview aliyofanya na jarida la Rolling Stone Breezy (24) aliielezea album hiyo kuwa imebeba nyimbo zinazohusu uzoefu wake binafsi na kuongeza kuwa hupenda kuchanganya uhalisia na sanaa.

Chris amesema mashabiki wake watarajie kusikia zaidi muziki wa live katika ‘X’ na watarajie kusikia matumizi madogo zaidi ya ‘auto tune’ sababu nia yake ni kuonesha uwezo wa sauti yake.

Kuhusiana na collabo yake na ex girlfriend wake Rihanna ‘Put It Up’, Breezy amesema bado hana uhakika kama itakuwepo ama haitakuwepo katika album hiyo, japo ipo katika orodha ya nyimbo wanazochagua kuingia katika album hiyo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents