Habari

COKE STUDIO AFRICA: Kipindi kipya cha TV cha muziki kinachowaunganisha wasanii bora 24 kutoka nchi 8 za Afrika

Kama wewe ni mtumiaji wa mitandao ya kijamii kuna uwezekano umeshakutana na picha za wasanii mbalimbali wa Afrika Mashariki wakiwa jijini Nairobi pamoja na mastaa wengine kutoka Afrika. Msanii wa hapa kwetu Lady JayDee alipost picha akiwa na Octopizzo wa Kenya, wakati Octopizzo pia aliweka picha akiwa na Fally Ipupa wa DRC, na Diamond PLatnumz pia alipost akiwa Coke Studio.

Coke studio

Coke Studio ni project kubwa ya vipindi vya muziki vya TV (Music television series) ambayo inasimamiwa na kampuni ya Coca Cola ambavyo tayari vimeshapata umaaraufu katika nchi za mabara mengine. Kabla ya kuja Afrika Coke Studio imefanywa katika nchi za Pakistan na India.

Vipindi hivyo uhusisha muziki uliorekodiwa live studio na wasanii mbalimbali maarufu kutoka sehemu mbalimbali na kuzirudia nyimbo zao kwa kuziboresha na kuzipiga kwa mitindo tofauti. Wasanii tofauti hukaa pamoja na kufanya kazi hiyo ya kurudia kuzitengeneza nyimbo hizo na kuzirekodi Live.

Diamond Coke Studio
Diamond Platnumz akiwa Coke Studio Nairobi

Coca Cola wamekileta Afrika kipindi hicho kinachoitwa COKE STUDIO AFRICA ambacho kitawaunganisha wasanii 24 kutoka nchi nane za Afrika, kwa mujibu wa ukurasa wa facebook wa Coke Studio Africa.

Lady JayDee & Fally
Lady JayDee akiwa na Falyy Ipupa

Bado haijawekwa wazi wasanii wote watakaohusika katika Coke studio Afrika lakini wale ambao tayari tunauhakika wa ushiriki wao ni pamoja na Diamond Platnumz na Lady JayDee kutoka Tanzania, Kutoka Kenya ni Octopizzo, Bamboo, Karun. Mastaa wengine ni Navio na Maurice Kirya kutoka Uganda, HHP na Mi Casa kutoka Afrika Kusini bila kumsahau Fally Ipupa kutoka DRC.

Octopizzo and Fally

Kipindi hicho kipya kitakuwa kikirushwa na TV ya Kenya NTV kila jumamosi kuanzia saa 2 usiku na pia kupitia QTV saa 3 usiku kuanzia tarehe 5 October mwaka huu.

Lady Jaydee & Octopizzo
Lady JayDee na Octopizzo
<img src="http://bongo5.com/wp-content/uploads/2013/09/Lady-JayDee-Lilian.jpg" alt="Lady JayDee & Lilian" width="960"

Wasanii 24 kutoka nchi 8 za Afrika watarekodi nyimbo 50 kwaajili ya kipindi hicho.

Tazama Promo ya kipindi hicho

http://youtu.be/mvouQ98bk6c

SOURCE: COKE STUDIO AFRICA

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents