Michezo

Confederation Cup 2017: Ronaldo atweta kwa Mexico, Cameroon hoi kwa Chile

Michuano ya kuwania kombe la mabara kwa ngazi za timu za taifa (Confederation Cup) imeendelea kutimua vumbi Jumapili hii huko nchini Urusi.

Katika mechi ya kwanza iliyochezwa katika uwanja wa Kazan Arena, iliwakutanisha kati ya Ureno na timu ya taifa ya Mexico ambao walitoka suluhu ya kufungana mabao 2-2. Magoli ya Ureno yalifungwa na Quaresma (34) na Cédric Soares (86), na magoli ya Urusi yalifungwa na Chicharito (42) na Moreno (90).

Katika mechi ya pili iliyochezwa katika uwanja wa Otkrytiye Arena, Cameroon walijikuta katika wakati mgumu baada ya kufungwa na Chile mabao 2-0. Magoli ya Chile yalifungwa na Vidal (81) pamoja na Vargas (90).

Mechi nyingine inatarajiwa kuchezwa Jumatatu hii katika uwanja wa Fisht Olympic, ambapo timu ya taifa ya Australia watacheza na Ujerumani.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents