Michezo

Coutinho ageuka lulu England, klabu 5 zapigana vikumbo, Pogba kutimka United ashindwe yeye tu

Katika kuhakikisha inaboresha kikosi chake, klabu ya Barcelona imemuweka sokoni kiungo wake raia wa Brazil, Coutinho ambaye tayari ameanza kuwaniwa na Manchester United, Liverpool, Chelsea, Manchester City na Tottenham.

Barcelona hatch £77m transfer plan as Man Utd, Liverpool and Chelsea eye Philippe Coutinho

Kwa mujibu wa mtandao wa Express Sport klabu hizo tano za Premier League zimenamtolea macho nyota huyo wa Barcelona aliyetokea Liverpool mwaka 2018

Coutinho amekuwa akihaha Barcelona lakini ameshindwa kwendana na kasi ya miamba hiyo ya Hispania na hivyo kupelekwa Bayern kwa mkopo.

Kiungo wa Manchester United na timu ya taifa ya Ufaransa Paul Pogba 26, milango ipo wazi kwa yeye kuomba kuondoka klabuni hapo mwishoni mwa msimu, wakati kandarasi yake mpaka sasa ikiwa imebaki miezi 12. (Manchester Evening News)

Manchester United pia wamepunguza makali yao katika kumfuatilia kiungo wa Leicester James Maddison, 23, ambaye anatarajiwa kuingia mkataba mpya na klabu yake. (Express)

Bayern Munich wanapanga kutoa dau la pauni milioni 75 ili kumnasa mchezaji wa wa Liverpool na Brazil, Roberto Firmino, 28, na pia wanataka winga wa Manchester City na timu ya taifa ya Ujerumani, Leroy Sane, 24, kuungana nae. (Sun)

Firmino

Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp anamfanya kiungo wa Bayer Leverkusen na Ujerumani Kai Havertz, 20, kama kipaumbele chake cha kwanza kwenye usajili wa mwisho wa msimu. (Express)

Klopp pia anapiga hesabu za kumrejesha Anfield kiungo wa Barcelona na Brazil Philippe Coutinho, 27, ambaye kwa sasa yupo kwa mkopo Bayern Munich. (Star)

Kipengele zha mauzo kwenye mkataba wa beki wa Napoli na Senegal Kalidou Koulibaly, 28, kitakuwa wazi kuanzia mwezi Juni kwa thamani ya pauni 127. Beki huyo amekuwa akihusishwa na uhamisho kwenda Man United. (Mirror)KoulibalyJe Man Uited kutoa zaidi ya pauni milioni 100 kumnasa Koulibaly?

Klabu ya Celtic ya Uskochi wanajipanga kumsajili mwishoni mwa msimu Josh Murphy, 24, kutoka klabu ya Cardiff baada ya kushindwa kumsajili mwezi uliopita. (Sun)

Kiungo wa Chelsea Italia Jorginho, 28, atakuwa mwenye furaha kuungana tena na kocha Maurizio Sarri Juventus, ameeleza wakala wake. (Mail)Andre OnanaAndre Onana

Kipa wa Ajax na Cameroon Andre Onana, 23, anatarajiwa kujiunga na Chelsea kwa dau la pauni milioni 34 mwishoni mwa msimu licha ya kuhusishwa na Barcelona na Paris St-Germain. (Caught Offside)

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents