Michezo

CV ya kocha wa Simba kiboko, apewa mkataba baada ya saa tano za mahojiano na jopo zito

CV ya kocha wa Simba kiboko, apewa mkataba baada ya saa tano za mahojiano na jopo zito

Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano Simba, Haji Manara amesema kuwa klabu hiyo ilipokea orodha ya makocha 57 waliyo kuja na kuomba kazi kabla ya Mbelgiji, Patrick Aussems kulamba dili hilo baada ya kufanyiwa mahojiano na  jopo la makocha na wataalam wakongwe kwenye soka kwa masaa matano.

Manara ameyasema hayo wakati wa akimtambulisha kocha huyo kwa waandishi wa habari jijini Dar es salaam hapo jana.

”Orodha ya makocha waliyo kuja na kuomba kazi Simba SC ni 57, kocha huyo amefanyiwa mahojiano kwa masaa matano. Kamati ya utendaji ya Simba ikateua jopo la makocha na wataalam wakongwe kwenye soka nchini kumfanyia mahojiano,” amesema Manara

Hata hivyo Manara ameelezea uzoefu wake ”Mbelgiji amefanyakazi kocha wa timu ya taifa ya Nepal, AC Leopards ya Congo, Al Hilal na timu ya taifa ya Benin.”

Kwa upande wake Mbelgiji kocha Patrick Aussems ameelezea namna alivyoipokea nafasi hiyo ya kukinoa kikosi cha mabingwa hao wa ligi kuu soka Tanzania Bara.

”Mimi ni kocha mpya wa Simba SC na najivunia kwa hilo kwasababu natambua klabu hii ni kubwa Tanzania yenye mashabiki wengi mno hivyo ni jambo muhimu kwangu kutafuta changamoto mpya,” amesema Aussems

Kocha mpya wa Simba Mbelgiji atua nchini kwa mara ya kwanza

Mbelgiji huyo ameongeza kuwa ”Mwezi uliyopita nilipata nafasi katika bara hili la Afrika lakini nikafanya maamuzi, nilipojua Simba ni klabu kubwa Tanzania hivyo nilihitaji kuifanya kuwa timu kubwa barani Afrika ndiyo maana nipo hapa.”

”Uzoefu wangu kama unavyouona nilikuwa Mkurugenzi wa ufundi wa timu ya taifa Benin na baadae nikawa kocha mkuu, nilikuwa AC Leopards ya Congo na kuifikisha nusu fainali ya kombe la Shirikisho Afrika na Al-hilal hivyo napenda kufanya kazi Afrika nilikuwa nasubiri nafasi hiyo nadhani nimepata hapa Simba na nipo tayari kuanza kazi yangu muda wowote.”

Mbelgiji huyo, Aussems anatuwa Simba huku akitarajia kukutana na kibarua kizito cha kutetea taji la ligi kuu na michuano ya kimataifa ikiwemo klabu bingwa barani Ulaya.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents