Michezo

David Moyes: Van Gaal anatakiwa apewe muda zaidi Man Utd

David Moyes amabye alikuwa Meneja wa zamani wa Manchester United amesema klabu hiyo kwasasa haifai kumfuta kazi Louis van Gaal licha ya klabu hiyo kuwa na matokeo mabaya.

3166D49800000578-0-image-a-176_1455994915972

Kumekuwa na taarifa kwamba klabu hiyo inajiandaa kumfuta kazi meneja huyo na kumpa kazi Mreno aliyefutwa kazi Chelsea mwezi Desemba Jose Mourinho.

Moyes, aliyefutwa kazi na klabu hiyo kufuatia kufanya vibaya na alidumu kwa miezi kumi pekee, amesema klabu hiyo haifai kupata sifa za “klabu inayofuta mameneja kiholela”.
Amesema ingawa klabu hiyo ilishindwa na klabu ya Midttyland FC ya Denmark katika mechi ya Europa Leauge Alhamisi, bado kuna mechi ya marudiano nyumbani ambayo wanaweza kushinda.
Moyes mesema alisikitika sana alipofutwa kazi baada ya kufanya kazi miezi kumi pekee.

Pia nyota wa zamani wa Newcastle United Alan Shearer amesema ni kama klabu hiyo haina matumaini tena hasa baada ya kushindwa 2-1 na Sunderland katika Ligi ya Premia.
Ameambia BBC Sport kwamba baada ya mechi hiyo, Van Gaal alionekana kama mtu aliyeishiwa na mawazo na aliyesalimu amri.
Kwa mujibu wa Shearer, uchezaji wao Europa League siku ya Alhamisi ulikuwa duni sana.

Source: BBC

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents