Burudani

Davido, wizkid na AKA wavuka mchujo wa kwanza kwenye kipengele cha ‘Best African Act’ tuzo za MOBO 2015

Mwanzoni mwa mwezi Octoba yalitangazwa majina ya wanamuziki wanaowania tuzo za ‘Music Of Black Origin’(MOBO) 2015 za Uingereza.

mobo

Katika tuzo hizo kipo kipengele kimoja cha wasanii wa Afrika ‘Best African Act’ ambacho kwenye hatua ya mwanzo kilikuwa na nominees 10.

Baada ya wiki moja majina hayo yalichujwa kutoka 10 na kubaki watano ambao ndio watakaochuana kupata mshindi mmoja wa kipengele hicho. Mchujo huo ulifanyika kwa kuangalia wingi wa kura za mwanzo.

Majina yaliyovuka mchujo wa kutoka 10 hadi 5 waliobaki ni Davido (Nigeria), Wizkid (Nigeria) , AKA (South Africa), Fuse ODG (British-Ghana) ,pamoja na Shatta Walle (Ghana) .

Majina yaliyokosa kura za kutosha na kuondolewa ni Yemi Alade (Nigeria) , Patoranking (Nigeria) , Moelogo (Nigeria) , Mista Silva (British-Ghana), Silva Stone (British- Sierra Leone & Ghana).

Hakuna msanii yeyote kutoka Afrika Mashariki aliyetajwa kuwania tuzo hizo za MOBO zitakazotolewa huko Leeds, Uingereza Novemba 4, 2015.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents