Diamond, Hamisa mmewafurahisha wambea – Haji Manara
Mara baada ya msanii wa Bongo Flava, Diamond Platnaumz kukiri kumtambua mtoto AbdulLatif wa mwanamitindo, Hamisa Mobeto kuwa ni wa kwake kupitia kipindi cha Leo Tena ya Clouds FM, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Klabu ya Simba, Haji S Manara ameingilia kati swala hilo kwa kumpakongole msanii huyo kukiri kuwa ni mwanawe.
Kupitia mtandao mtandao wake wa kijamii wa Instagram, Manara ameandika “Safi, umeongea kiume @diamondplatnumz”.
Ikiwa namaana ya kumsifu Diamond Platnaumz kwa kitendo alichofanya, Mkuu huyo wa Idara ya Habari ya Simba SC ameongeza kuwa “Diamond na Amisa leo mmewafurahisha sana wambeya!!naambiwa nchi nzima leo ilihamia clouds kusikiliza ubuyu,, Ubuyu oyeeeeee!!!@cloudstv @soudybrown@geahhabib“.
Diamond akiri mtoto wa Hamisa Mobeto ni wa kwake
Haya yamekuja mara baada ya msanii huyo akuweka bayana kuwahi kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mrembo huyo na mtoto AbdulLatif ni wake ila walikuwa na makubaliano ya kutotangaza katika mitandao.