Habari

Dodoma: Mambo 31 aliyozungumza Rais Magufuli wakati akifungua mkutano Mkuu wa chama cha Walimu

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo amezungumza mambo muhimu 31 wakati anafungua mkutano Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) mkoani Dodoma.

Baadhi ya mambo aliyoyazungumza Rais Magufuli ni kama ifuatavyo:

-Mimi ni mwalimu, sijabadilika, shida na raha za ualimu nazifahamu.

-Sisi vongozi ndani ya serikali hatuwezi tukawaangusha, walimu ni jeshi kubwa.

-Nashukuru Viongozi wa Chama cha Walimu kwa uamuzi wa kuufanyia Mkutano huu Mkoani Dodoma.

-Nitaendelea kuwa mtumishi wa watanzania wote,sitawabagua kwa Dini wala Vyama

-Sekta ya Elimu ni Nyeti na muhimu katika maendeleo ya nchi yoyote.

-Natoa pongezi kwa viongozi watangulizi wataifa hili kwa jitihada walizofanya katika kuiendeleza sekta ya elimu.

-Natoa pongezi kwa walimu kwa kazi kubwa mnayoifanya ya kuwaelimisha watanzania.

-Tumeongeza Fedha za elimu bure kutoka Tzs 18.77 Bil. Hadi kufikia Tzs Bil. 23.868 kwa mwezi na mpaka sasa tumetumia Tzs Bil. 535.

-Serikali ya Awamu Tano imejenga na kurabati shule za Msingi na Sekondari 365 mpaka sasa.

-Mwaka huu tumegawa vifaa vya maabara katika Shule za Msingi za sekondari 1696.

-Walimu wanapomaliza masomo wafanye kazi kwenye vituo wanavyopangiwa.

-Walimu wanaopewa Posho za Madaraka wazitumie vizuri, na wanaotoa madaraka watoe bila upendeleo kwa walimu wanaojituma kwa ajili ya watanzania.

-Serikali imelipa Tzs Bil. 56.92 kwa ajili ya kulipa madeni ya walimu.

-Haya Madeni ya walimu tutayalipa yote, mara baada ya kazi ya uhakiki wale wote walioomba madai halali watalipwa.

-Viongozi niliowateua akiwemo Makamu wa Rais ni watetezi wakubwa wa walimu.

-Tumeongeza bajeti katika sekta ya afya kutoka Tsz bil. 31 hadi Tzs Bil. 239.

-Mnapokaa katika vikao vyenu kumbukeni kuuliza madai ya fedha zenu ikiwemo kutoka Benki ya Walimu.

-Serikali inapaswa kuhakikisha kile kinachopatikana kinapelekwa katika sekta zote, kile kinacholetwa kwenu na serikali naomba mkipokee.

-Udahili wa wanafunzi umeongenzeka kutoka Mil. 1 hadi Mil. Moja na Laki 9 kutokana na elimu bure na kwa sekondari udahili umeongezeka kwa asilimia 31.

-Serikali imetoa ajira 3462 kwa walimu wa sayansi na niwaahidi walimu, wanafunzi ajira zipo.

-Mamlaka husika angalieni kwa makini suala la mgawanyo wa walimu Mijini na Vijijini, lakini isiwe mwanya wa kuhamisha bila kufuata utaratibu.

-Usihame kama hujalipwa pesa yako, hakuna atakayekufukuza kazi kama hajakulipa pesa ya uhamisho.

-Tumekuwa na hifadhi za Jamii nyingi zisizofuata taratibu za hifadhi za jamii, ndio maana tunataka tuwe nazo mbili, moja ya Serikali nyingine ya sekta binafsi.

-Tunataka tuwe na hifadhi za jamii zinazojali watu wake na zitakazojenga viwanda.

-Tunaziunganisha Hifadhi za sekta za jamii kwa lengo la kuboresha maslahi ya wafanyakazi.

-Natambua umuhimu wa posho ya kufundishia kwa walimu ili kuwapa motisha walimu

-Uchumi wa nchi yetu upo vizuri na ndio maana ipo miradi tunayoitekeleza kwa fedha zetu.

-Serikali inafahamu umuhimu wa kutoa mafunzo kwa walimu ili kuwaongezea uwezo.

-Katika uchaguzi wenu, msichague watu kwa maslahi yao wala kwa rushwa, viongozi watakaowapeleka mbele na kwa ajili ya maslahi ya walimu.

-Vyombo vya dola vinavyohusika na rushwa vinafanya kazi.

-Viongozi mliopo chambueni madai ya walimu katika mikoa yote na mkiridhika nayo yapelekeni kwa waziri mkuu, haiwezi kumaliza mwezi mmoja nitayalipa yote.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents