Burudani

Dogo Janja akingia kifua picha ya utupu ya Ben Pol

Wiki hii picha ya Ben Pol aliyopiga ikimuonyesha akiwa mtupu imeonekana kuteka hisia za watu wengi mitandaoni.

Picha hiyo ambayo alipost katika mtandao wake wa Instagram, imemsababishia kushushiwa mvua kubwa ya matusi kutoka kwa mashabiki lakini, msanii Dogo Janja ameonekana kuisoma picha hiyo kiundani zaidi.

Akiongea na kipindi cha 5selekt cha EATV Ijumaa, hitmaker wa “Ukivaaje Unapendeza?” amesema hawezi kumlaumu Ben labda alikosa nguo ya kuvaa katika picha hiyo ndio maana akaamua kufanya hivyo.

“Labda brother alijiuliza akivaaje atapendeza akaamua asivae kitu tu mbona fresh, lakini mimi sidhani kama nitaweza kufanya jambo kama lile kuwaonyesha watu. Too much hapana aisee vitu kama vile vinaishi milele. Unaweza kufanya leo ukapata maslahi lakini kesho kikawa na athari katika maisha yako,” amesema Janja.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents