Habari

Dr Rwakatare apigwa changa la macho

Watoto wawili wanaojulikana kwa majina ya Yusufu na Ramadhani wamelidanganya kanisa la Mikocheni B la Assemblies Of God lililo chini ya Mchungaji Dk Getrude Rwakatare, wakijifanya wamedondoka kutoka angani walikokuwa wakiwanga baada ya kuchukuliwa na wachawi

Dk Getrude Rwakatare

 

 

 

Watoto wawili wanaojulikana kwa majina ya Yusufu na Ramadhani wamelidanganya kanisa la Mikocheni B la Assemblies Of God lililo chini ya Mchungaji Dk Getrude Rwakatare, wakijifanya wamedondoka kutoka angani walikokuwa wakiwanga baada ya kuchukuliwa na wachawi lakini kutokana na maombi ya waumini wa kanisa hilo ndiyo yaliyowaoko na ndizo sababu zilizowapelekea wao kuwasili kanisani hapo.

 

 

 

Habari kuhusiana na utapeli wa watoto hao uliwahi kutangazwa na kituo maarufu cha runinga hapa nchini cha ITV ambapo ulithibitishwa na kamanda wa polisi wilaya ya kinondoni bwana Jamal Rwambow na kudai kuwa kabla ya kujifanya wameangukia katika kanisa hilo, siku chache zilizopita wamewahi kufanya tukio kama hilo huko maeneo ya mbezi tangi bovu mnamo januari 6 mwaka huu.

 

 

 

“baada ya polisi kupokea taarifa hizo za watoto hao, vijana wangu walifika katika eneo la tukio huko mbezi na kuwachukua mpaka katika kituo kidogo kilichoko maeneo ya kawe na kuwahoji kasha kuwapeleka hospitalini kwa ajili ya uchunguzi wa afya zao ambapo wauguzi waliwacheki na kugundua hawana maradhi yoyote na baada ya muda tulipokea taarifa kutoka kwa raia wanaowafahamu vijana hao zikidai kuwa hawana lolote ni matapeli kwani mwanzoni mwa Februari waliwahi kujifanya wameangukia huko maeneo ya Manzese kwenye noja ya makanisa ya maeneo ambapo walichukuliwa na kupelekwa katika moja ya vituo vya kulelea watoto yatima huko maeneo ya kurasini” alisema Kamanda Rwambow.

 
Kabla ya kuvuma kwa uzushi huo, watoto hao baada ya kubainika na kuwekwa hadharani kwa mara ya kwanza na ITV, waliueleza uongozi wa Kanisa la Mikocheni kuwa walikuwa wakiishi kama misukule katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam kwa muda mrefu sana.

 

 

 

Akizungumza na waandishi wa habari mchungaji Mama Rwakatare ambaye pia ni mbunge wa viti maalum (CCM), alisema kuwa watoto hao walidondoka wakati waumini wa kanisani hapo walipokuwa wakifanya maombi katika kumtukuza Mungu, alikaririwa akisema kuwa Watoto hao wanaokadiriwa kuwa na umri wa miaka kati ya saba na 10 waliamguka kutoka juu katika eneo la kanisa hilo baasa ya nguvu za giza kuelemewa kutokana na maombi ya kawaida ambayo huendelea ndani ya kanisa lake.

 
Siku kadhaa baada ya mkutano na waandishi wa habari, Mchungaji Dk. Rwakatare, alionekana tena kwenye luninga akiwa katika shughuli za kiroho na kuwahoji watoto hao waliodaiwa kudondoka kanisani hapo, huku wakidai kuwa walikuwa wakitokea Mwanza wakielekea Mtwara.
Akiwa na wachungaji wengine wa kanisa hilo, Dk. Rwakatare, aliwaombea watoto hao na kuwaeleza waumini wake kuwa, hayo ni matunda ya maombi yao na kwamba ‘Yesu wa kanisa lao’ anatenda miujiza.

 
Kwa muda mrefu sasa, kumekuwa na taarifa za watu wanaotuhumiwa kujihusisha na masuala ya kishirikina kudondoka kutoka angani kila mara wanapopita katika anga za baadhi ya makanisa nchini jambo ambalo kwa upande flani huashiria ni ishara moja wapo ya miujiza inayosababishwa na maombi ya waumini.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents