Burudani

Misoji ashinda BSS 2008!!

Hatma ya kinyang’anyiro cha kumsaka nyota wa bongo katika wasanii wanaochipukia Bongo Star Search, limekamilisha na mwanadada Misoji Nkwabi amesimikwa rasmi ushindi huo baada ya kuwazidi washiriki wengine watano amabo alikutana nao kwenye fainali hizo
Misoji Nkwabi

 

 

 

Hatma ya kinyang’anyiro cha kumsaka nyota wa bongo katika wasanii wanaochipukia Bongo Star Search, limekamilisha na mwanadada Misoji Nkwabi amesimikwa rasmi ushindi huo baada ya kuwazidi washiriki wengine watano amabo alikutana nao kwenye fainali hizo.

 

 

 

Tukio hilo lililofanyika ndani ya hotel ya Blue Pearl iliyopo ndani ya jingo la Ubungo Plaza jijini Dar Es Salaam Juzi usiku, lilihudhuriwa na maelfu ya watanzania ambao ndio waliopiga kura za kuchagua nani anastahili kuwa mshindi, Mwanadada Misoji aliweza kuchukua kitita cha fedha tasilimu shilingi milioni 18 na mizigo kibao ya mazawadi.

 
Shughuli hiyo ilihudhuriwa na Naibu waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo bwanaJoel Bendera, pia ilionekana kupambwa na wanadada mahiri kutoka nchini Jamaica Brick & Lace ambao waliweza kuzisuuza nyoyo za mashabiki waliokuwemo ukumbini humo na waliokuwa wakitazama majumbani mwao.

 

Brick & Lace

 
Licha ya kupewa Fedha Misoji alijinyakulia simu kutoka kampuni ya LG, Sofa seti toka the Living Room, TV, Gomputer, nafasi ya kusoma chuo cha uandishi wa Habari Times, ngazi ya Diploma pamoja na zawadi nyingine kem kem.

 

Unastahili Pongezi Misoji!

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents