Burudani

Dudu Baya ataka Amber Lulu na Gigy kuchukuliwa hatua kali za kisheria kabla 2018, kisa?

Msanii wa muziki wa Bongo Flava, Dudu Baya ameitaka serikali kupitia Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) kuwachukulia hatua wasanii wote ambao wameenda kinyume na maadali kwa mwaka 2017 ili mambo hayo yasije kujirudia mwaka 2018.

Dudu Baya akizungumza na E-Newz ya EATV amesema baadhi ya wasanii kwa mwaka huu wameitumia vibaya mitandao ya kijamii kwa kuweka picha zisizo na maadili kitu ambacho kimefanya jambo hilo kujadiliwa kuliko muziki wao.

“Watu kama kina Nuh Mziwanda wanapiga picha za uchi uko na Shilole kipindi kile uko bafuni unaoga kuna aja gani kuonyesha mashabiki wako, kuna mtu gani asiyeoga hapa duniani. Ukija kama suala la mdogo wangu Young Dee namkubali sana lakini alipiga picha na Amber Lulu za kumshika makalio, huo ni ujinga,” amesema Dudu Baya.

Dudu Baya ameendelea kwa kusema wasanii watumie mitandao kwa manufaa ya kibiashara na endapo wakishindwa basi sheria ichukue mkondo wake.

“Nabahatika nakutana na Amber Lulu au Gigy Money namwambia ebu kaza kwenye kipaji chako ebu achana na upuuzi, sasa hivi mabinti wanaotaka kuingia kwenye movie au muziki wasije kwa njia walizopitia Amber Lulu na Gigy,” amesema.

“Kama 2017 yamefanyika sana, ni serikali au Basata kuja na tamko, hao ni watu wa kutolea tamko atakayeenda kinyume basi sheria ifuate mkondo wake, siyo wakati wakuonyana ni wakati wa tamko kabla ya kuingia 2018,” amesisitiza.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents