Soka saa 24!

Elephant Man atua Bongo

elephant-man_face

Mwanamuziki mwenye machachari hasa kwa mtindo wa kupaka rangi nyekundu na njano katika nywele zake, toka nchini Jamaica, Elephant Man ametua jijini Dar es salaam kwa ajili ya Show kabambe itakayodondoshwa siku ya Jumamosi kando kando yaani fukwe za bahari Hindi pale Mbalamwezi Beach, katika bonanza la Str8 Music Beach Party.

Hii itakuwa ni historia nzuri kwa nchi ya Tanzania katika tasnia ya muziki kwa kudondosha wasanii wawili, yaani Shaggy na Elephant Man kutoka nchi moja na walizaliwa mji mmoja huko Kingston Jamaica, na kufanya show mbili tofauti ndani ya Tanzania kwa kupishana masaa kadhaa.

Shaggy atakuwa akitoa burudani ndani ya usiku wa Ijumaa pale Ngome Kongwe Zanzibar, katika tamasha la Filamu Zanzibar ‘Ziff’ wakati Elephant Man akitoa burudani jijini Dar es salaam pale Mbalamwezi siku ya Jumamosi usiku.

Hii inaonyesha wazi kwamba Tanzania sasa ipo juu kimuziki, na ndiyo maana hata wasanii wa nje hawahofiii katika masuala ya mapokezi na kutunzwa kwa heshima yao, kama Masuper Star.

Endelea kufuatilia hapa hapa Bongo5, uwe wa kwanza kujua wasanii toka nje watakao kuja kufanya Show, Serengeti Fisesta 2011.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW