Burudani ya Michezo Live

Elizabeth Michael ‘Lulu’ achaguliwa kuwa Balozi wa ‘Dar Filamu Festival’

Ikiwa ni wiki moja imepita toka mwigizaji mrembo wa Bongo Movie Elizabeth Michael aka Lulu azindue filamu yake ya ‘Foolish Age’ katika ukumbi wa Mlimani City, Dar es salaam milango yake ya mafanikio imeendelea kufunguka.

lulu4
Dar Filamu Festival Idara Habari Maelezo jana

Kupitia akaunti yake ya Instagram @Hotlulumichael, ameweka picha akiwa na waandaaji na kutoa shkurani zake kwa kuchaguliwa kuwa Balozi wa ‘Dar Filamu Festival’.

“Shukrani za dhati kwenu DAR FILAMU FESTIVAL kwa kunichagua kuwa BALOZI wenu(OFFICIAL ACTRESS 2013/2014)…”

Lulu kwa sasa anafanya shughuli zake za filamu chini ya kampuni ya Proin Promotions.

Dar Filamu Festival (DFF) ni tamasha la filamu linalotarajiwa kufayika kwa siku tatu kuanzia (September 24-26) katika viwanja vya posta-Kijitonyama, Dar es salaam. Kwa mujibu wa filamucentral, tamasha hilo litaambatana na utoaji wa Semina kwa wadau wa filamu, kuonesha filamu za kitanzania kwa watu wote bure na kutakua na filamu nne kwa siku kuanzia saa kumi na mbili jioni mpaka saa tano usiku.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW