Michezo

Fabregas, Alvaro Morata, Marcos Alonso na Bellerin watemwa timu ya taifa ya Hispania 

Wachezaji Cesc Fabregas, Alvaro Morata, Marcos Alonso, Ander Herrera na Bellerin watemwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Hispania kinachotarajiwa kwenda kushiriki michuano ya kombe la Dunia nchini Urusi mwaka huu.

Kocha wa timu ya taifa ya Hispania, Julen Lopetegui ametangaza majina ya wachezaji 23 watakao kuwemo kwenye kikosi kitakacho shiriki kombe la Dunia huku wanne wakitokea ligi kuu nchini Uingereza ambao ni David de Gea, Cesar Azpilicueta, Nacho Monreal na David Silva.

Kwakuwa Morata amekuwa akiangaika katika kuhakikisha anakuwa fiti tangu alipojiunga na Chelsea akitokea Real Madrid msimu uliyopita akiwa amefunga jumla ya mabao 11 tangua atue ligi kuu ya Uingereza.

Wakati, Andres Iniesta amejumuishwa kwenye kikosi baada ya kucheza mchezo wake wa mwisho ndani ya klabu yake ya Barcelona.

Kikosi kamili cha timu ya taifa ya Hispania kitakachoshiriki kombe la dunia mwaka huu hiki hapa.Walindalango ni David de Gea, Pepe Reina, Kepa Arrizabalaga

Mabeki ni Dani Carvajal, Alvaro Odriozola, Gerard Piqué, Sergio Ramos, Nacho, Cesar Azpilicueta, Jordi Alba, Nacho Monreal

Viungo wa kati ni  Sergio Busquets, Saul, Koke, Thiago Alcantara, Andres Iniesta, David Silva

Na safu ya ushambuliaji ni  Isco, Sergio Asensio, Lucas Vazquez, Iago Aspas, Rodrigo, Diego Costa

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents