Fahamu ahadi ya Morrison kwa Bosi wa Simba kupitia mazungumzo yao ya simu

Mchezaji mpya wa Simba SC, Bernard Morrison ameweka wazi alicho ahidi mbele ya bosi wa klabu hiyo kupitia mazungo yake kwa njia ya simu.

Morrison ameandika alicho ahidi kwa bosi huyo kuwa atakuwa mfano bora, mwenye heshima kwa klabu na wanachama wake huku akihakikisha kufanya kazi kwa juhudi zote ili kuwapa furaha wana Msimbazi.

”Nimemaliza mazungumzo na Bosi wa Simba SC kupitia simu na nimemuahidi kuwa mfano bora, kuheshimu klabu na wanachama wake na kufanya kazi kwa bidii ili kila mmoja afurahi.”- Amesema Bernard Morrison

Morrison ameongeza kuwa ”Kuna wengine nilifanyanao kazi miezi minne tu, kitu pekee walichogundua kwangu mimi ni kijana mbaya, mara moja nilitaka kuachana nao, walichogundua kwangu ni kuwa sina nidhamu nilipohitaji kuondoka.”

”Sikuwa na tatizo na mtu yoyote, kwenu ninyi mashabiki wa Simba, nimekuja hapa kukaa, nipo hapa kuwafanya mfurahi, nipo hapa kuheshimu na kuwawakilisha kwa njia yoyote ile.”

Simba ilimtambulisha rasmi Bernard Morrison wikiendi iliyopita huku sajili yake ikigubikwa na utata hali iliyopelekea kuamuliwa na Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW