Michezo

Fahamu sababu za Griezmann kutokuvaa jezi 7 msimu mzima, licha ya kuipenda na mwenye namba yake kuondoka

Mchezaji mpya wa Barcelona, Antoine Griezmann aliyesajiliwa kutoka Atletico Madrid ili kurithi nafasi ya Mbrazili, Coutinho kwa mara ya kwanza ameitumikia timu yake siku ya Ijumaa huku akiwa amevalia jezi namba 17 mgongoni badala ya (7) ya Philippe ambayo yeye anaipenda zaidi.

Antoine Griezmann is stuck with the No 17 shirt despite Philippe Coutinho going out on loan

Griezmann ataendelea kuvaa jezi 17 na kamwe hatoichukua namba saba (7) anayoipenda licha ya mmiliki mwenywe, Philippe Coutinho kuondoka Barcelona na kujiunga na miamba ya soka ya Ujerumani, Bayern Munich kwa mkopo.

Kwa mujibu wa sheria za shirikisho la soka nchini Hispania, La Liga linasema kuwa mchezaji atalazimika kuendelea kubakia na namba ya jezi yake aliyoanza kuitumia kwenye mechi rasmi mwanzoni mwa msimu na kudumu nayo mpaka mwisho wa msimu bila kubadilisha.

A player must wear the same number throughout the season, so Griezmann can't get No 7 yet

Kama dili la Coutinho kusajiliwa kwa mkopo Bayern lingetimia mapema kabla ya mechi za msimu kuanza, basi Mfaransa huyo, Griezmann angeweza kuvaa jezi namba saba (7) ambayo anaipenda kuitumia.

Bayern imemchukua Coutinho kwa mkopo kutoka Barcelona huku dili hilo likiwa na kipengele cha kumnunua moja kwa moja kwa dau la Pauni Milioni 110 kama miamba hiyo ya soka kutoka chini Ujerumani itahitaji kufanya hivyo.

Image result for Griezmann atletico

Griezmann alivyokuwa Atletico Madrid akiwa amevalia jezi namba 7

Matumaini ya Griezmann kuvaa jezi namba saba (7) ni mpaka msimu ujao wa ligi. Hata hivyo nyota huyo hakuwa na mwanzo mzuri kwenye timu yake mpya baada ya kushuhudia Barcelona ikipokea kipigo cha bao 1 – 0 kutoka kwa Athletic Bilbao huku yeye mwenyewe kiwa miongoni mwa wachezaji waliyokuwa uwanjani.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents