MichezoUncategorized

Fainali ya NBA: Golden State Warriors yaendelea kuinyanyasa Cavaliers

Golden State Warriors imeendelea kuinyanyasa Cleveland Cavaliers katika fainali ya tatu ya mchezo wa kikapu wa NBA.

Katika mchezo huo uliochezwa alfajiri ya kuamkia leo katika uwanja wa Quicken Loans Arena, Golden wameshinda kwa jumla ya vikapu 118 dhidi ya 113 vya Cleverland.

Mchezaji Kevin Durant ameendelea kuwa nyota wa fainali hizo baada ya kufanikiwa kushinda pointi tatu zikiwa zimebakia sekunde 45 za mchezo huo kumalizika.

Kwa sasa unasubiriwa mchezo wa mwisho utakaochezwa wikiendi hii ambapo kama Golden atashinda tena ndio atakuwa bingwa mpya wa mchezo huo kwa mwaka huu ambao msimu uliopita ulinyakuliwa na Cleveland Cavaliers.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents