Michezo

Fainali ya NBA: Golden State Warriors yaendelea kuinyanyasa Cavaliers

Golden State Warriors imeendelea kuinyanyasa Cleveland Cavaliers katika fainali ya tatu ya mchezo wa kikapu wa NBA.

Katika mchezo huo uliochezwa alfajiri ya kuamkia leo katika uwanja wa Quicken Loans Arena, Golden wameshinda kwa jumla ya vikapu 110 dhidi ya 102 vya Cleverland.

Mchezaji Kevin Durant amefanikiwa kuwa nyota wa fainali hiyo baada ya kufanikiwa kushinda pointi 43 huku kwa upande wa Cavaliers, LeBron James ndio alikuwa nyota kwa kupata alama 33.

Fainali nyingine inatarajiwa kupigwa Juni 9 ya mwaka huu katika uwanja wa Quicken Loans Arena. Mpaka sasa Warriors wamefanikiwa kushinda michezo mitatu mfululizo ya fainali huku Cavaliers wakiwa hawajashinda hata mchezo mmoja.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents