Habari

Foxy Brown: Sijawahi kusema kuwa Jay-Z ana ‘kisonono’

Rapper wa kike wa siku nyingi ambaye pia ni muigizaji na model, Foxy Brown amekuja juu baada ya baadhi ya vyombo vya habari kuandika madai kuwa alisema Jay-Z ana maambukizi ya kisonono.

foxy-image

Ripoti iliyoandikwa na baadhi ya vyombo vya habari zinasema kuwa Brown alihudhuria katika ‘baby shower’ moja na kuanza kuzungumzia mahusiano ya kimapenzi ya Jigga kwa mmoja wa wageni, akimwambia kuwa amewahi kujihusisha kwa siri na ushoga na kuwa yeye ndiye aliyemtoa bikra akiwa na miaka 15 wakati huo Jay akiwa na miaka 27.

Akizungumza na mtandao wa TMZ, Brown mwenye asili ya mchanganyiko wa Trinidad na Asia ameonesha kukerwa mno na habari hizo na kukanusha kwa kusema, ‘katika miaka yangu yote kwenye muziki, haya ndio madai ya kunikosea heshima ambayo sikuwahi kupata, na hii ni habari ya uongo ambayo haina uthibitisho wa sauti, video wala interview ya maandishi na hivyo ina dhamira ya uongo.”

Jay z n foxy

Aliendelea kupinga kwa kusema kuwa, “Jay amekuwa mtu mzuri sana kwangu na familia yangu, rafiki mzuri katika miaka yote niliyomfamahu na hatukuwa na chochote zaidi ya mafanikio kama team.”

“Beyonce mke wake amekuwa mtu mzuri sana kwangu, siwezi kuruhusu undercover hater asababishe ugomvi na kuniharibia jina na sifa yangu.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents