Michezo

Froome atwaa taji la Vuelta a Espana

Bingwa wa dunia mara nne wa mbio za Baiskeli za Tour de France, Chris Froome amefanikiwa kushinda taji la Vuelta a Espana kwa mara yake ya kwanza toka alipoanza mchezo huo baada ya kuibuka wa kwanza katika mashindano hayo Jijini Madrid nchini Hispania hapo jana siku ya Jumapili.

Froome mwenye umri wa miaka 32, amekuwa mshiriki wa kwanza kushinda Hispania na watatu katika historia ya mashindano hayo kutwaa mataji mawali ya Vuelta na the Tour de France ndani ya mwaka mmoja.

Mwendesha Baiskeli huyo mzaliwa wa Jiji la Nairobi nchini Kenya na kukulia Afrika Kusini huku wazazi wake wakiwa ni raia wa Uingereza aliweza kufanikiwa kumshinda bingwa mara nne wa Grand Tour, Vincenzo Nibali kwa kumzidi dakika mbili na sekunde 15 katika michuano hiyo.

Mara kadhaa, Froome amekuwa akimaliza katika nafasi ya tatu katika mashindano hayo ya La Vuelta ikiwemo mwaka jana lakini amekuwa na mafanikio makubwa msimu huu baada ya kamera kunasa akikimbia kilomita 117.6 katika hatua ya mwisho ya mashindano hayo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents