Burudani

FUNGUKA NA MUUMINI vs BANZA STONE

BONGO5

Kwanza samahani, wadau wa Bongo5!! Tulileta kwenu utambulisho tulioufanya mwanzo kwamba ukurasa huu, tutaanza kuuweka kila jumamosi na hatamaye kuja leo siku ya jumapili tena jioni.

Hii ilitokana na sababu ambazo zipo nje ya uwezo wetu, lakini nadhani mambo yatakuwa sawa zaidi na kuendelea na elimu yetu juu ya sanaa na mazingira yote yanayotuhusu sisi watanzania.

Bado tunarudia lengo lipo pale pale kwamba tutoe elimu ya ukweli ili tuwewe kuendelea, pia kwenye kukosoa tukosoa bila kuogopa, na kwenye kueleza ukweli tueleze bila ya kusita, kwani ukweli unauma ila unaponya, pia tunaruhusu kutoa mifano ya watu mbalimbali, ilianayehusika ajifunze na tunarusu kutoa maoni na nani tumuongee kwa wakati ujao, na kwanini?

KWA kuaza na mada yetu, nadhani huu utakuwa muda mzuri kwa kuzungumzia kujadili na kuelimishana kuhusiana na wanamuziki wa bendi za dansi kupoteza majina yao kwa haraka huku wakihama kila siku kutoka bendi moja au nyingi.

Kibaya zaidi kuhama huko hakujulikani kama kimasirahi, ama ndiyo fahari wawili…..

.,banzabc

LEO…Tunaye Ramadhani Masanya maarufu kama Banza Stone, ambaye kwa sasa safari yake imetua Extra Bongo, baada ya kuzunguka bendi tofauti na ya mwisho ni Rufita Connection aliyohama Juzi….

muumini

MWINGINE… Mwijuma Muumini, ambaye naye hana tofauti kati yake na  Banza Stone, alihama bendi nyingi na hata kufikia kuanzisha bendi yake ya Bwagamoyo na hatmaye mambo yamekuwa si mambo na sasa yupo African Stars ‘Twanga Pepeta.

Je? Kuhana huko, wewe unafikiria nini, Je tunakuza muziki wetu, Maslahi madogo wanayopata, wamiliki wa bendi ndiyo tatizo au unafikiri nini kinasababisha? Kazi kwako

 

 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents