Burudani

ASET yamuondoa ADOLPH MBINGA Twanga

Adoph_Mbinga

UONGOZI wa ASET umemuondoa ndani ya Bendi ya African Stars “Twanga Pepeta”  mwanamuziki  Adolph Mbinga kutokana na kutokutimiza wajibu wake ndani ya Bendi kama ilivyotarajiwa wakati akijiunga na Twanga Pepeta mwishoni mwa mwaka jana.


Kuanzia tarehe 15-05-2011 yuko huru kujiunga na Bendi yeyote atakayoona inamfaa na kwa upande wa Twanga Pepeta tumeanza mchakato wa kumtafuta Mpiga gitaa mwingine ili kuziba nafasi yake iliyoachwa wazi. Kwa sasa tuna wapigaji gitaa mahiri waliobaki ambao ni wa siku nyingi ndani ya Bendi ambao ni  Miraji Shakashia “Shakazulu”, Jumanne Said Mkandu “Jojoo Jumanne”, Kado Hassan na Godfrey Kanuti.

Adolph Mbinga hakuwa na Mkataba wowote na ASET ila alikuwa kwenye kipindi cha uangalizi maalum kabla ya kuingia mkataba na ASET lakini ameshindwa kuonyesha maendeleo yeyote toka anaingia kwenye Bendi mpaka tulipoamua kumuondoa kwenye Bendi.

Kwa muda wote aliokuwa ndani ya Bendi alikuwa akilipwa stahili zote alizopaswa kulipwa kama tulivyokubaliana naye kabla ya kuingia ndani ya Bendi.

ASET bado inathamini mchango wa ADOLPH Mbinga ndani ya Twanga Pepeta kwa kuwezesha kutunga nyimbo zilizoipa umaarufu Bendi ya African Stars wakati inaanza kabla ya kutimkia Mchinga Sound  pale alipodiriki kujaribu kuondoka na takriban wanamuziki 6 muhimu waliokuwa wakiunda Twanga Pepeta, lakini kwa sasa hatutoweza kuwa naye baada ya kushindwa kumudu aina ya muziki wa sasa Twanga Pepeta inaoupiga na kushindwa kutimiza wajibu wake ndani ya Bendi.

MARTIN SOSPETER

MENEJA WA BENDI.

 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents