Burudani

Godzilla adai Hip Hop ya Tanzania imekosa ushindani ‘rappers wamekalia kubishana’

Msanii wa Hip Hop kutoka pande za Salasala, Godzilla amesema kuwa game la wasanii wa Hip Hop kwa sasa halina ushindani ukilinganisha na ushindani uliopo kwa wasanii wa kuimba.
1

Akizungumza kwenye The Hot Seat ya kipindi cha The One Show, cha TV1 ,Godzilla amedai kuwa wasanii wa Hip Hop sasa hivi wamebase kwenye kubishana kuliko kutengeneza kazi nzuri.

“Watu unajua wanaandika vizuri, lakini sehemu moja tunakosea, game letu halina ushindani,naamini tumewapa nafasi sana watu wa kuimba. Yaani ukifanya Hip Hop watu wanasema achana na ngumu wewe imba. Kwa mfano ukienda unyamwezini watu wanatembeza track dizaini fulani kama akina Rozay hivi. Ukitengeneza track unaweza ukapiga club, unaweza ukapiga radio. Sisi watu wanatengeneza Hip Hop fulani hivi imekuwa huwezi cheza club. Kwahiyo huwezi shindana air play na watu wa kuimba, hata ukienda Bilicanas, unaweza ukasikiliza nyimbo kumi za watu wa kuimba lakini unaweza kutengeneze Hip Hop fulani ambayo hata club zitachezwa. Lakini kama tumekwama sehemu, watu wamebase kwenye kubishana wakiacha kutengeneza kazi za kumove. Wasani wanaofanya Hip Hop nzuri ya commercial wapo mainstream. Watu wengine wamebase kwenye ku criticize, wengine hawana taaluma wanakosoa tu.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents