Burudani

Young Killer: Namkubali Bow Wow, siku moja naamini ntafanya naye kazi

Ndoto za rapper mshindi wa msanii chipukizi wa tuzo ya KTMA 2014 Young Killer Msodoki ni kufanya kolabo na msanii mkali wa Marekani Bow Wow.

Young Killer akikabidhiwa JB  tuzo ya msanii bora chipukizi KTMA 2014
Young Killer akikabidhiwa JB tuzo ya msanii bora chipukizi KTMA 2014

“Kiukweli kabisa mimi nampenda Bow Wow, Bow Weezy namkubali. One day naamini nitafanya nae kazi, mwenyezi Mungu akijalia nikipata nafasi nitafanya nae kazi,” Young Killer ameiambia tovuti ya Times FM. Young Killer aliendelea kuelezea mambo ya muziki ambayo alikuwa anayafikiria kabla ya kufika hapo halipo.

“Yaani kabla hata sijatoka nilikuwa nimeshafikiria ila naamini kila kitu kinakuja na wakati. Hatua moja huanzisha nyingine, leo nimepata tuzo kesho kitu kingine kitafanyika na kesho kutwa kitu kingine kitafanyika. Kwa hiyo nina dream ya kufanya kazi na watu wengi sana kwa hiyo naamini nitafanikiwa tu, kama hiki pia nilikiomba kimefanikiwa naamini hata hicho kingine kitakuja.”

Source:Tovuti ya Times Fm

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents