Awards

Grand Gold Award Yatua Bongo Kwa Mbwembwe

Bia ya Ndovu Special Malt inayozalishwa na Kampuni ya Tanzania Breweries Limited Jana iliwasili nchini Tanzania ikitokea jiji la Wiesbaden nchini Ujerumani ambako ilikabidhiwa tuzo kubwa ya dhahabu inayokwenda kwa jina la Grand Gold baada ya kuzibwag zaidi ya aina 2000 za bia zinazozalishwa katika nchi mbalimbali duniani.

Bia hiyo ya Ndovu Special Malt imekuwa bia ya kwanza nchini na katika ukanda wa Afrika Mashariki kufanikiwa kutunukiwa tuzo ya hali ya juu katika shindano la World Monde Selection 2010 liliofanyika.

Akizungumza na waandishi wa Habari baada ya kutua toka Ujerumani meneja wa bia hiyo bwana Oscar Shelukindo alisema bia hiyo ya …imefanikiwa kushinda tuzo ya ubora wa juu kabisa baada ya jopo la wataalamu wa vinywaji ulimwenguni kupitia ki umakini vinywaji mbali mbali vilivyokuwa katika ushindanishwaji huo.

Nae mpishi mkuu wa biawa Tanzania Brewaries Limited (TBL) BwanaGaudence Mkolwe alisema tuzo ya Grand Gold iliyopata Bia ya Ndovu Special Malt ni uthibitisho wa kutosha wa ubora wa bia zinazotengenezwa na kamuni hiyoya bia hapa nchini,

Mashindano hayo yaliyokutanishazaidi ya vinywaji 2000 toka kampuni mbalimbaliulimwenguni, yanasimamiwana wataalamu waliobobea katika utengenezaji wa vinywaji, ambao hupitiakinywaji kimoja baada ya kingine na kw kutumia vifaa bora vya kisasa kupima ubora wa vinywaji hivyo.

Nae mkurugenzia wa Masoko wa kampuni hiyo TBL Bwana David Minja alisema mafanikio ya bia hiyo ya ndovu Specia Malt ni mwendelewzo wa mikakati ya kampuni hiyo katika kuwapatia wanywaji vinywaji bora na kwa kuishinda tuzo hiyo TBL imedhihirisha umakini na ubora wa vinywaji vyake ambapo ni jambo la kujivunia katika jamii yetu,

Baada ya kutoka katikauwanja wa ndege tuzo hiyo ya Grand Gold ilipelekwa katika makao makuu ya kiwanda kinachozalishwa bia hiyo eneo la Ilala Karume barabara ya Uhuru ambapo mkurugezi mtendaji wa Kampuni hiyo bwana alisifia mafanikio hayo na kuwataka wafanyakazi kuendeleza ubora wa bidhaa hiyo na nyinginezo zinazozalishwa kiwandani hapo.

Jioni ya jana tafrija nyingine iliandaliwa katika viwanja vya hoteli y Movenpick jijini dar-Es-salaam ambapo sherehe rasmi ya kuitambulisha tuzo hiyo kwa wadau na wanywaji wa kinywaji hicho ilifanyika.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents