Michezo

Guardiola: Ningeshatimuliwa kama ningekuwa Barcelona ama Bayern Munich

Meneja wa klabu ya Manchester City , Pep Guardiola, amesema kama angekuwa katika klabu ya Barcelona ama Bayern Munich basi angekuwa ameshafukuzwa kwa kumaliza msimu bila taji lolote.


Meneja wa Manchester City , Pep Guardiola

City, imeshindwa kunyakuwa taji lolote msimu huu ikiwa chini ya Meneja Guardiola ambaye ndio msimu wake wa kwanza. Pamoja na hilo, bado pia inakosa uhakika wa kumaliza nafasi nne za juu katika msimamo wa Ligi huku ikiwa imesalia na michezo miwili kabla ya Ligi kumalizika.

Lakini pia kwa upande wake, Guardiola, ameshuhudia mataji yakimpita yakiwemo klabu bingwa barani ulaya akitolewa katika hatua ya 16 bora, Kombe la FA akitolewa katika hatua ya nusufainali pamoja na kombe la ligi akitolewa katika hatua ya nne.

“Katika mazingira haya,katika klabu kubwa kama hii ningekuwa nimeshafukuzwa”,. Nisingekuwepo tena,” Alisema Mhispania huyo.
“Kama ingekuwa ni Barcelona na Bayern hujashinda taji usingekuwepo tena”.Hapa nina nafasi nyingine na nitajaribu kufanya vyema katika msimu mpya utakapo anza”

Klabu hiyo inayoongozwa na Matajiri wa mafuta ‘Waarabu’ italazimika kushinda michezo yake yote miwili iliyosalia ili kujihakikishia kuwa katika nafasi ya nne juu ya klabu za Liverpool na Arsenal, ili iweze kushiriki michuano ya klabu bingwa barani ulaya msimu ujao.

Kiungo huyo wazamani wa Barca mwenye umri wa miaka,46, aliipatia klabu ya Barca mataji 14 katika miaka 4 tu aliyo ka hapo kama Meneja, ikiwemo na mataji matatu ya La Liga na mawili ya klabu bingwakati ya mwaka 2008 pamoja na 2012.

Baada ya kuchukua mapumziko ya mwaka mzima alijiunga na klabu ya Bayern Munich ya nchini Ujerumani mwaka 2013 na kushinda taji la Bundesliga kwa misimu mitatu mfululizo ndani ya dimba la Allianz Arena.

Bayern pia ilishinda taji la Ujerumani kwa misimu miwili mfululizo, lakini, Guardiola , hakusalia katika klabu hiy mara baada ya kutolewa tu katika nusu fainali ya klabu bingwa barani Ulaya.

BY HAMZA FUMO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents