Tupo Nawe

Haina jinsi, Juan Cuadrado akabidhi jezi kwa mwenye namba yake

Baada ya kukamilika kwa uhamisho wa Cristiano Ronaldo kutua klabu ya Juventus, mashabiki wa Turin wanahitaji mchezaji huyo kukabidhiwa jezi ya namba yake halisi.

Katika zoezi hilo la jezi anaepoteza zaidi ni kiungo wa Colombia, Juan Cuadrado ambaye anavaa namba saba kabla ya ujio wa Ronaldo.

Mcolombia, Juan Cuadrado kiroho safi amekubali kumuachia jezi hiyo mchezaji mpya wa Juventus, Cristiano Ronaldo baada ya kuandika kwenye mtandao wake wa Twitter kuwa ni heri kumkabidhi. ”Ni vema zaidi kutoa kuliko kupokea,” amesema Cuadrado.

Cristiano Ronaldo mwenye umri wa miaka 33 amejiunga na Juventus ya nchini Italia juzi kwa dau la pauni milioni 105 akitokea Real Madrid.

Ronaldo ambaye ni mshindi mara tano wa Ballon d’Or ametumia misimu tisa Madrid baada ya uhamisho wake wa pauni milioni 80 akitokea Manchester United huku akiondoka na kuwacha rekodi ndani ya klabu hiyo kwa kufunga jumla ya mabao 451.

Nahodha huyo wa Ureno ameondoka Real baada ya kushinda mataji mawili ya La Liga titles, mawili Copa del Rey na mataji manne ya klabu bingwa barani Ulaya.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW