Michezo

Hamilton ashinda Singapore GP, Vettel akipata ajali (Video)

Dereva maarufu wa magari ya Mercedes, Lewis Hamilton amekuwa bingwa wa mbio za Singapore Grand Prix baada ya kumshinda mpinzani wake, Sebastian Vettel kutoka timu ya magari ya Ferrari hapo jana siku ya Jumapili.


Hamilton ameshinda ubingwa huo wa mbio za Formula One ‘F1’ wa Singapore huku akikosa upinzani kutoka kwa Vettel ambaye alipata ajali mapema baada ya gari lake kugongana na la dereva mwenzake ambaye wote wanatokea timu moja ya Ferrari.

Katika duru ya tano ya mbio hizo, Hamilton ameonekana kusuasua na kufanikiwa kukaa sawa na kuongoza baada Vettel kugongana na Kimi Raikkonen.

Mara baada ya ushindi huo, Lewis Hamilton amesema kuwa alitambua kama angeshinda michuano hiyo ya Singapore GP baada ya kubadilika kwa hali ya hewa na kunyesha kwa mvua.

https://www.youtube.com/watch?v=PC_rDz21_uc

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents