Michezo

Harry Kane afikia rekodi ya Steven Gerrard EPL

Straika wa klabu ya Tottenham, Harry Kane ameibuka mchezaji bora wa mwezi Disemba wa ligi ya England na kuwa sawa na kiungo wa Liverpool, Steven Gerrard  kwa kuchukua mara sita tuzo hiyo.

Straika wa klabu ya Tottenham, Harry Kane

Kane amefunga jumla ya mabao nane katika michezo sita aliyocheza ukiwemo na ule wa Burnley na Southampton.

Kwa kutwaa tuzo hiyo sasa anakuwa sawa na kiungo wazamani wa Liverpool na nahodha wa timu hiyo Steven Gerrard.

Kane amesema kuwa anajisikia furaha kutwaa tuzo hiyo na atahakikisha anafanya vema katika mchezo wao ujao wikiendi hii dhidi ya Everton.

Kiungo wazamani wa Liverpool na nahodha wa timu hiyo Steven Gerrard.

Miongoni mwa wachezaji waliyokuwa wakiwania tuzo hiyo ya mwezi Disemba ni pamoja na winga wa Chelsea, Marcos Alonso, Marko Arnautovic, Roberto Firmino na Mohamed Salah, Jesse Lingard wa Manchester United, Riyad Mahrez na beki wa Manchester City, Nicolas Otamendi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents