Michezo

Hassan Isihaka kuikabili derby ya Sukari Mtibwa V Kagera

Beki kisiki wa wana tam tam aliyekuwa anasumbuliwa na majeraha yaliyomuweka  nje kwa takribani miezi mitatu, Hassan Isihaka amesha anza mazoezi na wenzake na yupo tayari kwa derby Mtibwa Sugar dhidi ya Kagera Sugar , mtandao wa klabu www.mtibwasugar.co.tz  umezungumza na daktari wa Mtibwa, Mussa Juma ili kutaka kujua hali za kiafya za wachezaji  katika timu ilivyo kwa sasa.

“Hali ni shwari katika timu wote wako sawa kikubwa ni kurudi kwa Hassan Isihaka na tumemruhusu kufanya mazoezi ya kila aina na ni ruksa kutumika katika mchezo wowote,” amesema daktari Juma.

Mussa Juma ameongeza “Majeruhi waliobaki kwa sasa  ni Haruna Chanongo, Shaban Kado na Salum Kanoni, na hawa watakosekana katika mchezo ujao dhidi ya Kagera ” Juma

Kikosi cha wana tam tam kinaendelea na mazoezi yake katika uwanja wake wa nyumbani chini ya mkufunzi wake mkuu Zuber Katwila “Puchetino” kikijiwinda kwa ajili ya mchezo dhidi ya Kagera Sugar.

 Rekodi za Head to Head

Kuelekea mchezo huo wa Jumapili ya November, 9 rekodi baina ya timu hizi mbili zinapokutana uwanja wa Manungu , katika michezo saba  iliyopita Mtibwa Sugar wamefanikiwa kushinda  michezo 5 na kutoka sare 2 na hawajapoteza dhidi ya Kagera katika uwanja wao wa nyumbani.

Mchezo wa mwisho kuchezwa katika uwanja wa Manungu baina ya timu hizi mbili ilikuwa  September 17,20016  Mtibwa Sugar ilifanikiwa kuwanyuka Kagera Sugar 2-0 , magoli ya Mtibwa Sugar yalifungwa na Ibrahim Rajab “Jeba” na Haruna Chanongo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents