Michezo

Hawa ni wachezaji walionekana hawafai na sasa wamekuwa lulu kwenye timu zao

Bahati ya mwenzio usiilalie mlango wazi. Kuna wachezaji wengi ambao wanaonekana hawafai kwenye timu zao lakini wanapoenda kwenye timu zingine nyota zao zinaanza kung’aa na kuzitoa udenda timu zao zilizowatema.

14Mesut-Ozil-1

Kwa sasa ukiambiwa list ya wachezaji kumi ambao unawakubali hakika kwenye list hii hutaacha kuwataja wachezaji hawa ambao walionekana ni mizigo kwenye timu zao hapo mwanzo.

Romelo Lukaku

450038_heroa

Romelo Lukaku, ni mchezaji wa Everton ambaye ni raia wa Ubelgiji. Mwanzoni Lukaku (22) alionekana kuwa mzigo kwenye timu yake ya Chelsea, tangu amesajiliwa August 2011 na timu hiyo, Lukaku aliichezea mechi 15 tu timu ya Chelsea pasipo kufunga goli hata moja.

Nyota ya Lukaku ilikuwa mbaya kwani tangu alipojiunga na Chelsea alijikuta akitolewa kwa mkopo kwenye timu nyingine, 2012-2013 alitua West Bromwich Albion kawa mkopo, aliichezea timu hiyo mechi 35 na akafanikiwa kuifungia magoli 17 timu hiyo.

Msimu wa 2014-2015 alipelekwa tena kwa mkopo kwenye timu ya Everton ambapo ndani ya misimu hiyo aliweza kucheza mechi 81 na kufanikiwa kufunga magoli 36. Julai 30, 2015 timu ya Everton walitangaza rasmi kumsajili Lukaku ada ya uhamisho wa paundi milioni 28. Tangu asajiliwe rasmi na Everton, Lukaku, amefanikiwa kucheza mechi 36 na kufunga magoli 25.

Lukaku ameonyesha thamani yake wikiendi iliyopita, Everton waliifunga Chelsea kwa magoli mawili kwa bila kwenye kombe la FA, magoli yote ya Everton yalifungwa na Lukaku.

Poul Pogba

Pogba

Tarehe 15 Machi, 1993 ni siku ambayo alizaliwa mchezaji wa Juventus, Poul Pogba. Pogba alionekana ni mchezaji wa kawaida sana alipokuwa anaichezea Manchester United. Alijiunga na academy ya Manchester United Oct 7, 2009. Mechi yake ya kwanza kuichezea timu ya wakubwa ya United ni Januari 31, 2012 ilikuwa dhidi ya Stock City, alichukua nafasi ya Chicharito dakika ya 72. Pogba aliichezea mechi saba United lakini hakufanikiwa kufunga goli lolote.

Mchezaji huyo kuonekana kuwa na mchango wowote chini ya kocha Alex Ferguson, Julai 3 timu ya Juventus ilimsajili mchezaji huyo kama mchezaji huru. Nyota ya Pogba haikamatiki kwa sasa kwani tangu amesajiliwa na mabingwa hao wa Italia ameshacheza mechi 168 na kufanikiwa kufunga magoli 60.

Kwa sasa timu kubwa kama, Real Madrid, Barcelona, Manchester City na Manchester United zinamfukuzia mchezaji huyo ambaye ni mmoja kati ya viungo bora duniani kwa sasa.

Philippe Coutinho

article-2632605-1D14AE7B00000578-206_634x415

Nchi ya Brazil imebarikiwa sana kuwa na wachezaji wenye vipaji vya dunia. Phillipe Coutinho ni mmoja kati ya wachezaji wenye umri mdogo lakini wamebarikiwa kuwa na vitu vikubwa wakiwa uwanjani. Jina la Coutinho limefahamika zaidi pale aliposajiliwa na majogoo hao wa Liverpool kutoka Inter Milan kwa thamani ya paundi milion 8.5.

Countiho alionekana kuwa ni mmoja kati ya wachezaji wasiokuwa na lolote kwenye timu ya Inter Milan. Tangu asajiliwe na Inter Milan msimu wa 2010-2013 alifanikiwa kucheza mechi 47 na kufunga magoli matano.

Julai 30, 2013, timu ya Liverpool ilitangaza rasmi kumsajili mchezaji huyo na mechi yake ya kwanza ilikuwa dhidi ya West Bromwich Albion. Aliingia dakika ya 78 kuchukua nafasi ya Stewart Downing.

Mpaka sasa Coutinho ameichezea Liverpool mechi 131 na amefunga magoli 23, tangu amejiunga na Liverpool nyota ya Coutinho imezidi kung’aa na ameonekana kuwa muokozi kwenye timu hiyo ambayo haionekani kufanya vizuri kwenye ligi.

Mesut Ozil

14Mesut-Ozil-1

Ukiulizwa taja viungo watatu bora duniani jina la Ozil halitakosa kwenye list yako. Mesut Ozil (27) alikuwa na wakati mgumu chini ya kocha Jose Mourinho wakati anaifundisha timu ya Real Madrid.

Ozil alijiunga na Real Madrid, Agosti 17, 2010 kwa kiasi cha Euro milioni 15 akitokea timu ya Werder Bremen. Mechi ya kwanza kwa Ozil kuichezea timu ya Madrid ni Septemba 15, ilikuwa dhidi ya Real Mallorca walipotoka sare ya bila kufungana, Septemba 13 alitoa assist yake ya kwanza kwa Higuan kwenye mechi ya Uefa dhidi ya Ajax.

Ozil ameichezea Madrid jumla ya mechi 159 na kufanikiwa kufunga magoli 27, msimu wa mwaka 2013-2014 ulikuwa mbaya sana kwa Ozil alicheza mechi mbili tu na hakufanikiwa kufunga goli hata moja.

Septemba 13, 2013 timu ya Arsenal walimsajili Ozil kwa dau la paundi milioni 50 akiweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza wa timu hiyo kusajiliwa kwa dau kubwa kama hilo. Kwa sasa Ozil amekuwa ni lulu kwenye timu ya Arsenal akiwa tayari ameshaichezea mechi 108 na amefunga magoli 19. Pia Ozil ameweka rekodi ya kuwa na assist 20 akiivunja ile ya Henry ya assist 18.

Mpaka sasa Ozil ndio mchezaji bora wa Ujerumani, amechukua tuzo hiyo mara tatu mfululizo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents