Burudani

Hii ndio kauli ya Barakah The Prince kwa wanafunzi wanaopata mimba shuleni

Msanii Barakah The Prince amefunguka baada ya kauli ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli siku chache zilizopita wakati akiwa katika ziara yake katika Mkoa wa Pwani juu ya wanafunzi watakaopata mimba wakiwa shuleni.

Rais Magufuli alisema katika wa utawala wake hakuna mwanafunzi atakayepata mimba na kuruhusiwa kurudi shule. Kutokana na kauli hiyo Barakah ameiunga mkono lakini amemtaka Rais kuangalia upya kauli yake hiyo juu ya wanafunzi hao wa kike na badala yake wanaume wanaowapa mimba watoto hao ndio wapewe adhabu kubwa zaidi.

Akiongea na Bongo5, hitmaker huyo wa Acha Niende amesema,“Japo kuwa ni kweli hawa mabinti wakiwa wanarudi shule itakuwa ni system sasa ya mabinti wote kubeba ujauzito kwa kuwa anajua hata nikibeba mimba nitakaa miezi tisa tu halafu nitarudi darasani. Hiyo ya kufukuzwa shule na asirudi kabisa hilo ni funzo lakini sidhani kama ni plan ya Mhe. Rais, lakini itakuwa ni fundisho na itawafanya watu wawe makini.”

“Watanzania tunaishi katika mazingira magumu sana ujue, mtoto katoka kwao kapewa labda shiingi 500 tu ya nauli na hata hajui atapataje breakfast shuleni halafu anaenda anakutana na vijamaa wanampa shilingi 50,000 au laki, wanamshawishi mtoto wa watu anajikuta anaingia kwenye hayo mambo. Hawa jamaa ambao ndio kishawishi kikubwa kwa hawa wanafunzi inabidi wachukuliwe hatua kali sana,” ameongeza.

Wakati huo huo muimbaji huyo amesema yeye hajawahi kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mwanafunzi katika maisha yake.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents