BurudaniMichezo

Hussein Machozi: Mashabiki msimu ujao wataniona kupitia soka, najiandaa kusajiliwa na Kagera Sugar

Muimbaji wa bongo fleva Hussein Rashid Dodi a.k.a Hussein Machozi, ametangaza kuwa mwakani (2016) huenda ukamuona akiingia uwanjani kuichezea timu ya soka ya Kagera Sugar katika Ligi kuu Tanzania Bara msimu ujao.

machozi-2

Akizungumza kupitia kipindi cha ‘Hatua Tatu’ cha Times Fm, Machozi amesema kuwa kwa sasa yuko kwenye mazoezi makali kujiandaa kusajiliwa na timu hiyo.

“Nipo mazoezini sasa hivi kwa ajili ya kujiandaa na kusajiliwa na Kagera Sugar kwa ajili ya kuichezea msimu ujao, so mazoezi wanakuja wananitazama kila siku, kwa hiyo mashabiki watambue msimu ujao wataniona kupitia soka”

Kabla ya kuanza safari yake ya muziki , kipaji cha kwanza cha staa wa ‘Kwaajili Yako’ kilikuwa ni kucheza mpira.

Source: Times FM

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents