Burudani

Idadi ya tattoo alizonazo Vanessa Mdee

Msanii wa Bongo Flava, Vanessa Mdee a.k.a V Money ametaja idadi ya tattoo zilizopo katika mwili wake.

Vanessa ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake mpya ‘Kisela’ aliyomshirikisha Mr P wa kundi la P Square ameiambia show ya The Playlist ya Times Fm kuwa ana tattoo zipatazo nane.

“Nina tattoo nane, zina maana tofauti tofauti, kuna nyingine zipo hapa ndani kwenye vidole, kuna nyingine hapa mguuni, kuna nyota, kuna switch hapa ambayo mimi na Mimi Mars tunayo, ni kama switch za ukutani lakini kila time ipo on, unajua Mungu alikuwasha so no one can switch off,” amesema Vannessa.

By Peter Akaro

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents