Habari

Ipad Art: Picha ya Morgan Freeman iliyochorwa kwa kidole kwa kutumia Ipad, ni ngumu kutofautisha na halisi (Video/Picha)

Msanii wa kuchora kutoka Uingereza ameonesha umahiri wa kipaji chake kwa kuchora picha kwa kidole kwa kutumia Ipad, ambayo kwa haraka haraka unaweza kushindwa kutofautisha na halisi na picha halisi aliyoi copy.

Kyle Lambert (26), amewashangaza watu wengi baada ya kuchora picha za muigizaji maarufu wa Hollywood, Morgan Freeman, ambayo kama wewe sio mtaalam wa kuchunguza picha unaweza usijue ipi ni halisi na ipi ni ya kuchora, tena kwa kidole kwenye Ipad.

Ip-1
Hii ni picha iliyochorwa na Lembert kwa kidole kwenye Ipad
Ip-2
Hii ni picha halisi ambayo Lambert aliiangalizia

Kwa kujua kuwa atakutana na maswali ya wengi watakaoshindwa kuamini kama kweli picha hiyo ni ya kuchora, msanii huyo ameambatanisha picha hiyo na video kionesha hatua zote wakati wa kuchora picha hiyo kuanzia mchoro unapoanza hadi mwisho.

Video hiyo ambayo imewekwa youtube jumatatu (December 2), imeshatazamwa mara 5,153,101.

Picha halisi ya Morgan Freeman, ambayo Lambert ameitumia kui copy, ilipigwa na mpiga picha aitwaye Scott Gries.

Ip-3
Hatua za awali
Ip-4
Kwa mbaaali lakini bado

Lembert alitumia app maalum ya kuchora iitwayo Procreate. Picha hiyo ilimchukua Lambert masaa 200 ndani ya mwezi mzima mpaka kuikamilisha.

Ip-5
Okay! Tunaelekea lakini bado
Ip-6
Almost there
Ip-7

Ip-8
Na hii ndio picha iliyochorwa na Lambert kwa kidole kwenye Ipad, ikiwa imekamilika

Hata hivyo picha ya Freeman sio picha pekee ambayo msanii huyo amechora, zipo picha za watu wengine maarufu akiwemo Beyonce pamoja na Rihanna, zote zikiwa zimechorwa kwa kidole katika Ipad.

Ip-9
Hii ni picha ya Beyonce aliyoichora kwa Ipad mwaka 2010 wakati anaanza kukionesha kipaji chake

Ip-10

Lembert amekuwa akitumia Ipad kuchora toka 2010.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents