Michezo

Iran : Kwa mara ya kwanza Wanawake waruhusiwa kuingia viwanjani kushabikia soka

Wanawake nchini Iran wameruhusiwa kuhudhuria mechi ya mpira wa miguu mjini Tehran kwa mara ya kwanza baada ya takribani miaka 40.

Wanawake 3,500 walihudhuria mechi ya kufuzu kwa kombe la dunia mjini Tehran

Wanawake walipigwa marufuku kuingia kwenye viwanja vya mpira wa miguu tangu mwaka 1979 baada ya mapinduzi ya Kiislamu.

Hatua hiyo ilichukuliwa kufuatia kifo cha shabiki aliyejichoma moto baada ya kukamatwa kwa kuhudhuria mechi ya soka.

Lakini shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu limetaja hatua hiyo ya siku ya Allhamisi kama ya njama kujipatia “umaarufu”.

Shirika hilo linasema mashabiki wanawake walitengewa “tiketi chache ” na kutoa wito marufuku dhidi yao kuondolewa.Wanawake wa Iran wakiishabikia timu yao wakati wa mechi za kufuzu kwa kombe la dunia

Zaidi ya wanawake 3,500 walinunua tiketi ya kuhudhuria mechi ya kufuzu kwa kombe la dunia kati ya Iran na Cambodia, ambapo walipewa nafasi ya kukaa sehemu maalumu iliyotengea wanawake pekee katika uwanja wa Azadi Stadium ambao unaweza kuhimili jumla ya watu 78,000.

Tiketi za wanawake ziliripotiwa kuisha dakika chache baada ya kutolewa.

Picha kutoka ndani ya uwanja huo zinaonesha mashabiki wa kike waliojawa na furahawakipeperusha bendera ya Iran wakishangilia timu yao.Mashabiki wa soka wa Iran wakiishabikia timu yao kabla ya mechi ya kufunzu ya kombe la dunia

Suala la ubaguzi wa kijinsia katika soka ya Iran liligonga vichwa vya habari duniani mwezi uliopita baada ya shabiki wa kandanda Sahar Khodayari, maarufu “blue girl” kujichoma moto nje ya mahakama akisubiri kesi dhidi yake kwa kuhudhuria mechi kinyemela akijifanya kuwa mwanamume.

Mwanamke huyo wa miaka 29 alifariki dunia wiki moja baadae.

Shirikisho la soka duniani Fifa imekuwa ikishinikiza Tehran kuwaruhusu wanawake kuhudhuria mechi ya kufuzu kwa kombe la dunia

Lilisema wiki hii kuwa ita simama “kidete”kuhakikisha wanawake wanapewa nafasi ya kuhudhuria mechi za soka nchini Iran.

Saudi Arabia mwaka jana iliruhusu wanawake kwa mara ya kwanza kuhudhuria mechi ya mpira wa miguu kama sehemu ya kulegeza sheria kali ya kutenganisha wanawake na wanaume katika nchi hiyo ya Waislamu wa kihafidhina.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents