Burudani

Iyo afunguka anavyomkubali Diamond na sababu ya kumshirikisha kwenye ‘Loving You’ (video)

Iyo kutoka Nigeria amefunguka jinsi anavyokumkubali Diamond na sababu iliyompelekea kumshirikisha kwenye wimbo wake ‘Loving You’ ambao umempatia umaarufu mkubwa.

Mpaka sasa wimbio huo umeshafanikiwa kutazamwa mara 1.2 milioni kwenye mtandao wa Youtube tangu ulipotoka mwezi Disemba mwaka jana. Muimbaji huyo ameimabia Bongo5 kuwa Diamond ni msanii mzuri na ni mkubwa Afrika ndio maana aliamua kumshirikisha kwenye wimbo huo.

“Mara tu niliposikia ule wimbo kiukweli nilikuwa studio kwa Masterkraft alicheza mdundo (beat) niliupenda haraka nikarekodi kiitikio nikapenda kuwa na Diamond katika wimbo huo. Nilijua tu kwamba mimi sikuwa na uwezo wa kuwa na uhusiano na msanii mwingine, Diamond ni mtu mwenye kuheshimiwa kwa muda mrefu,” amesema Iyo.

“Mimi ni heshima kumekuwa na kuheshimiwa kwa muda sana kwa muda mrefu sana. Mimi ni shabiki mkubwa sana wa Diamond, hivyo ilikuwa ni ndiyo kama ungeniuliza Diamond niamini na jamaa ni msanii wa ajabu kwanini asiwe yeye? Lakini pia ni maamuzi sahihi ambayo nimewahi kuyatoa, yeah kweli kabisa,” ameongeza.

Iyo amesisitiza kwa kusema, “Diamond ni msanii mzuri sana na ni mkubwa siyo Afrika Mashariki kama unavyojua ni mkubwa Afrika na kiukweli anakwenda kimataifa haraka sana kama unavyojua, akili yake ipo haraka sana na ninafikiria kila mtu anapenda kumshirikisha mtu kama yeye na kama unavyojua sikutarajia nipependa hiki kitu, kwahiyo Diamond ni kitu kizuri kwanini tusikate keki?”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents