Burudani

Baby J kufanya party ya uzinduzi wa Foundation yake pamoja na kutangaza ujio wake mpya

Msanii wa muziki kutoka visiwani Zanzibar Baby J Machi 18 anatarajia kufanya party maalumu kwajili ya uzinduzi wa Foundation yake mpya ambayo itakuwa inajihusisha na kuwasaidia wasanii.

Muimbaji huyo ameiambia Bongo5 kuwa party hiyo itahudhuriwa na wadau mbalimbali wa muziki pamoja viongozi wa serikali.

“Hiyo siku kuna na mambo mengi yatafanyika kuhusu muziki wangu, ni siku maalum kwangu ambayo nitangaza mambo mengi kuhusu muziki wangu, kwa hiyo wadau wangu wakae tayari kwajili ya ujio mpya wa Baby J nimejipanga vizuri kwajili ya mwaka 2017. Tunafanya corporate dinner ambayo itakua ni launch ya Baby J Foundation kwa lengo la kuwasaidia wasanii wachqnga wanaochipukia hasa wasanii wa kike na pia itakua inafanya kazi ya kusaidia kuibua vipaji vipya vya wasanii wa kike Zanzibar.

Aliongeza, “Kwa muda ambao nimekaa kwenye game nimeshuhudia matatizo makubwa wanayowapata wasanii wachanga wanapoanza hasa wa kike. Wasanii wangapi hawana elimu ya kujua ugumu wa kuwa msanii, so nataka foundation yangu iwe inasaidia kuwajengea uwezo wasanii wanaonza na kuwapa awareness ya ambacho watakaja kukabiliana nacho kwenye game,”

Party hiyo imepangwa kufanyika Maruhubi Beach Villa, Maruhubi kuanzia saa moja usikui

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents