Jack Wilshere aikacha Arsenal kiaina na kutua West Ham United 

Aliyekuwa mchezaji wa klabu ya Arsenal, Jack Wilshere amejiunga na timu ya West Ham United  kwa kandarasi ya miaka mitatu.

Wilshere mwenye umri wa miaka 26 amekamilisha safari ya miaka 17 aliyotumikia Arsenal toka alipojiunga mwaka 2008.

Baada ya kujiunga na wagonga nyundo hao wa Uingereza, Wilshere ameiyambia tovuti ya West Ham kuwa anajiskia vizuri na kama mtu maalum.

Huku kiungo huyo akiongeza kuwa watu watarajie kuona picha yake kwenye uzi wa West Ham na kukumbushia namna anavyokumbuka akiisapoti klabu hiyo alivyo kuwa mdogo wakati akiifuatilia.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW