DStv Inogilee!

Jaffary Kibaya atupia ‘hat trick’ na kuibeba Mtibwa Sugar  CAF Confederation Cup

Klabu ya Mtibwa Sugar imefanikiwa kuibuka na ushindi wa jumla ya mabao 4 – 0 dhidi ya Nothern Dynamo ya Usheli Sheli mchezo uliyopigwa uwanja wa Azam Complex wa Chamazi.

Kwenye mchezo huo wa kwanza wa michuano ya Shirikisho Afrika ( CAF Confederation Cup), Mtibwa imechomoza na ushindi huo baada ya dakika 45 za kwanza kutoka na mabao mawili kisha na kumalizia mengine mawili katika kipindi cha pili.

Nyota wa mchezo huo hii leo alikuwa ni Jaffary Kibaya wa Mtibwa Sugar baada ya kupiga ‘hat trick’ na kuondoka na mpira wa mtananfe huo huku Riphat Msuya akihitimisha karamu ya magoli kwenye dakika za nyongeza kabla ya mpira kumalizika.

Hapo kesho mashabiki wa soka watashuhudia klabu ya Simba ikiingia uwanjani kuiwakilisha Tanzania katika michuano ya klabu bingwa Afrika itakapo wakabili Mbabane Swallows kuanzia saa 10:00 jioni.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW