Habari

Janeth Jackson na mumewe wana mpango wa kuasili mtoto Syria ama Jordan

Yalianza mapenzi, ikafuata ndoa, na sasa anatafutwa mtoto ili kuikamilisha familia yao mpya mwimbaji Janeth Jackson na mumewe mfanyabiashara billionea Wissam Al Mana wa Qatar.

Janeth na mumewe

Kwa mujibu wa US Weekly chanzo kimoja kimethibitisha kuwa Janeth (47) anafanya utafiti wa kimya kimya juu ya taratibu wa kuasili mtoto kutoka nchi ya dunia ya tatu.

Habari zaidi zinasema kuwa pop star huyo amemfuata Queen Rania wa Jordan ili amsaidie kumuwezesha kuasili mtoto.

Janeth Jackson ambaye ni mke wa Wissam Al Mana walianza uhusiano (2010 na baadaye kufunga ndoa. Al Mana ni mume wa tatu kwa Janeth ambaye hapo kabla alikuwa ameshaolewa mara mbili.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents