AFCON 2019 Tupogo!
Vodacom Data Datani!

Jay-Z aachia wimbo wa kwanza ’Holy Grail’ katika albam yake mpya ‘MCHG’ iliyoachiwa leo kwa watumiaji wa Sumsung

Hatimaye dini la kwanza kutoka katika mgodi wa ‘Magna Carta Holy Grail’ wa Shawn Carter limedondoshwa rasmi leo (June 4). Ladies and gentlemen, here comes the hip hop mogul Jay-z in his latest joint ‘HOLY GRAIL’ akiwa amempa shavu Justin Timberlake katika chorus.

Jay z cover

Huu ni wimbo wa kwanza kutoka katika album ya ‘Magna Carta Holy Grail’ ambayo imekuwa na maandalizi makubwa sana pamoja na promo ya kutosha katika kipindi cha wiki mbili za mwisho kabla ya siku ya kutoka.

Kwa mujibu wa vyanzo vya mtandaoni usiku wa kuamkia leo (July 4) imefanyika party ya siri ya kusheherekea kutoka kwa album hiyo iliyohudhuriwa na watu wa karibu bila kusahahu mke, Beyonce pamoja na mmoja wa maproducer wa album hiyo Timberland.

Kama ilivyokuwa imetangazwa awali wateja milioni 1 wa Samsung wenye bahati walidownload album nzima katika simu zao na watu wengine wataipata albam hiyo, July 7 (mitandao mingine imeandika itatoka July 9) itakapotoka rasmi kwa watu wote.

Single ya kwanza kutoka katika album ya ‘MCHG’ ambayo Timberland anaita kuwa ni “best album ever” ilitambulishwa kwa mara ya kwanza kupitia kituo cha radio Hot 97 usiku wa kuamkia leo.

P. Diddy ni moja kati ya watu walio tweet juu ya album ya Hov kwa kusema Jay Z ameweka historia na kuipa shavu kwa kuipromote album hiyo katika akaunti yake ya twitter.

Usikilize wimbo huo mpya ‘Holy Grail’

[soundcloud url=”http://api.soundcloud.com/tracks/99610755″ params=”” width=” 100%” height=”166″ iframe=”true” /]

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW