Burudani

Jay Z sasa ni wakala rasmi wa wachezaji wa Basketball (NBA) na Baseball (MLB)

Star na mfanyabiashara mwenye mafanikio makubwa ndani na nje ya kazi za muziki Shawn Corey Carter maarufu zaidi kama Jay Z, hatimaye ameidhinishwa na kupewa leseni kuwa wakala rasmi wa wachezaji wa baseball (MLB) pamoja na basketball (NBA).

Jay Z

Jana Alhamisi (June 20) chama cha Baseball (Major League Baseball Players Association)
kimethibitishia mtandao wa USA Today kuwa sasa Jay Z anauwezo wa kufanya maelewano ya mikataba ya wachezaji wa baseball kwasababu amekuwa wakala rasmi.

Upande mwingine msemaji wa Roc Nation Sports Ron Berkowitz, amethibitisha kuwa Jay Z ameidhinishwa na ‘National Basketball Players Union’ kufanya kazi kama wakala wa wachezaji wa basketball, taarifa ambayo pia mara ya kwanza ilitolewa na Sports Business Journal.

“Shawn ‘Jay-Z ‘ Carter submitted an application to the NBA league office to sell his interest in the Brooklyn Nets and our review process is underway, “Our rules prohibit an NBA owner from having businesses that represent NBA players. Jay-Z has been certified as an NBA player agent by the NBPA, and upon successful completion of the transfer of his ownership interest, there will be no prohibition from him representing NBA players.”

Sasa hip hop mogul Jay Z akiwa kama wakala rasmi anauwezo wa kumfanya ‘Robinson Cano’ kuwa maarufu kama alivyoimba katika verse ya pili ya wimbo wake wa ‘Empire State of Mind’ aliomshirikisha Alicia Keys, “I made the Yankee hat more famous than a Yankee can”. Cano ndiye mteja wa kwanza wa Jay Z toka aingie katika biashara ya michezo kama wakala.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents