Michezo

Jezi mpya Man United zazua gumzo

Miamba ya soka nchini England Manchester United wamezitambulisha Jezi zao za tatu zitakazo tumika msimu wa 2020/21.

Jezi hizo zenye muonekano wa Punda milia zimepokelewa katika mitazamo tofauti na mashabiki wa Mashetani hao Wekundu wa England.

Licha ya baadhi ya wachezaji wa kikosi cha kwanza cha United kutumika katika kuitangaza Jezi hiyo akiwemo, Bruno Fernandez, Marcus Rashford na Scott McTominay lakini pia aliyekuwa mchezaji nyota wa klabu hiyo na mfanyabiashara, David Beckham ameonekana kuvalia uzi huo.

Mashabiki wanadai kuwa hazina muonekano mzuri wengine wakisema “Hata Beckham zimemfanya kutokuwa na muonekano mzuri. ” – Mcasemarcus shabiki

Prateek yeye ameandika ” Msajilini Sancho na sisi tuta wasamehe kuhusiana na hiyo jezi yenu ya tatu”.

Luis Parker “Watu wataitumia jezi hii kukatiza Barabarani. ”

Reddevil76 “Kamwe sitaandika jina langu katika jezi hii ya kuzalilisha hatakama nitaipata bure. ” Hayo ni maoni machache katika yale mengi yaliyotolewa na mashabiki wa United.

IMEANDIKWA NA HAMZA FUMO, INSTAGRAM @fumo255

 

https://www.youtube.com/watch?v=–8_K8i_n90

https://www.youtube.com/watch?v=mkdIZEWJvrY

https://www.youtube.com/watch?v=RqlNWL0C0rE

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents