Michezo

Jonas Mkude kulipwa mamilioni Simba Sc

Baada ya vuta nikuvute ya Klabu ya Simba na Nahodha wao Jonas Mkude kuhusu kuongeza mkataba sio siri tena kuwa mchezaji huyo atasalia klabuni hapo na atakuwa ndiyo mchezaji anaepokea mkwanja mrefu kuliko wote klabuni hapo kwa mwezi.
Jonas Mkude
Habari za uhakika kutoka ndani ya Simba zinaeleza kuwa Mkude atalipwa kiasi cha Shilingi milioni 5 za kitanzania kwa mwezi nje ya malupu lupu na posho ambazo watalipwa endapo timu yake itafanya vizuri.
Mkude ambaye wiki hili kuliibuka Sintofahamu baada ya tetesi kutoka kwa watu wake wa karibu wakidai kuwa huenda akaihama klabu hiyo endapo hawatamuongezea mshahara amesaini mkataba wake mpya na Simba SC jana na kuzima matumaini ya Klabu ya Yanga ambao walikuwa wanawinda saini yake.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents