Juma Mahadhi aibeba Yanga SC Vs St Louis klabu bingwa Afrika

Mchezaji wa klabu ya Yanga, Juma Mahadhi ameisaidia timu yake kuibuka na ushindi wa bao 1 – 0 dhidi ya St Louis mchezo wa klabu bingwa Afrika raundi ya kwanza ulipigwa uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Katika mchezo huo uliyokuwa na ushindani wa aina yake kikosi cha klabu ya Yanga kimefanikiwa kutawala mchezo huo katika kipindi cha kwanza kwa wastani wa asilimia 78 dhidi ya 22 za timu ya Louis licha kutoka sare katika kipindi hicho cha kwanza.

Katika kipindi hiko chwa kwanza straika wa Yanga SC, Obrey Chirwa ameshindwa kuipatia bao timu yake baada ya kukosa penati ambayo imetokana na mchezaji Hassan Kessy kufanyiwa mazambi katika eneo la hatari.

Mchezaji Juma Mahadhi amefanikiwa kuipatia bao timu hiyo wakati wa kipindi chapili baada ya kuchukua nafasi ya Ibrahim Ajib aliyekwenda benchi.

Kwa matokeo hayo sasa timu hizo mbili zinatarajiwa kukutana tena mchezo wa marudiano baada ya wiki moja huko Shelisheli.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW